Surah Quraish

Listen

Swahili

Surah Quraish - Aya count 4

لِإِیلَـٰفِ قُرَیۡشٍ ﴿١﴾

Kwa walivyo zoea Maqureshi,

Hebu staajabuni kwa yanayo walazimu Makureshi! Kuwalazimu safari za musimu wa baridi kwenda Yaman,


Arabic explanations of the Qur’an:

إِۦلَـٰفِهِمۡ رِحۡلَةَ ٱلشِّتَاۤءِ وَٱلصَّیۡفِ ﴿٢﴾

Kuzoea kwao safari za siku za baridi na siku za joto.

Na safari za musimu wa joto kwenda Shamu, kufanya biashara na kutafuta riziki kwa utulivu na amani. (Hizo safari za biashara za Yaman ndizo zilizo waleta Waarabu Afrika Mashariki kwa maelfu ya miaka, na zikauleta Uislamu pande za Afrika kabla ya kuenea Arabuni. Kwani nchi za Afrika Mashariki zilikaliwa na Waarabu kwa maelfu ya miaka. Soma Periplus of the Erythrean Sea, na East Africa and Its Invaders ya Prof. Coupland, na vitabu vya Sir John Gray na Dr. L.W. Hollingsworth.)


Arabic explanations of the Qur’an:

فَلۡیَعۡبُدُواْ رَبَّ هَـٰذَا ٱلۡبَیۡتِ ﴿٣﴾

Basi nawamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii,

Basi wamtakasie ibada Mola Mlezi wa Nyumba hii aliye wawezesha kuzifanya hizi safari mbili.


Arabic explanations of the Qur’an:

ٱلَّذِیۤ أَطۡعَمَهُم مِّن جُوعࣲ وَءَامَنَهُم مِّنۡ خَوۡفِۭ ﴿٤﴾

Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na khofu.

Ambaye anawalisha wasione njaa, na hali wao wamo katika bonde lisio na makulima, na akawalinda na khofu na watu wengine pembezoni mwao wananyakuliwa.


Arabic explanations of the Qur’an: