Surah Al-Mu'minoon (The Believers)

Listen

Swahili

Surah Al-Mu'minoon (The Believers) - Aya count 118

قَدۡ أَفۡلَحَ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ﴿١﴾

HAKIKA wamefanikiwa Waumini!

Kumethibiti kufanikiwa kwa Waumini wanao muamini Mwenyezi Mungu na waliyo kuja nayo Mitume; na wamefuzu kwa wayatakayo.


Arabic explanations of the Qur’an:

ٱلَّذِینَ هُمۡ فِی صَلَاتِهِمۡ خَـٰشِعُونَ ﴿٢﴾

Ambao ni wanyenyekevu katika Swala zao!

Hao ambao wameambatisha juu ya Imani yao vitendo vyema. Basi hao katika Swala zao humuelekea Mwenyezi Mungu kwa nyoyo zenye kumkhofu na kumnyenyekea, wanahisi unyenyekevu wa mwisho kwake Yeye .


Arabic explanations of the Qur’an:

وَٱلَّذِینَ هُمۡ عَنِ ٱللَّغۡوِ مُعۡرِضُونَ ﴿٣﴾

Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi!

Hao wanashughulikia mambo ya maana, wanapuuza vitendo na maneno yasiyo na kheri ndani yake.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَٱلَّذِینَ هُمۡ لِلزَّكَوٰةِ فَـٰعِلُونَ ﴿٤﴾

Na ambao wanatoa Zaka!

Nao wanashikilia kutoa Zaka kuwapa wanao stahiki. Kwa hivyo wanakusanya ibada ya mwili na ibada ya mali, na baina ya kujisafisha nafsi na kuyasafisha mali. "Na ambao wanatoa Zaka,": Huu waajibu wa kutoa Zaka unapelekea kujenga mashikamano ya umoja baina ya Waislamu, na kutia katika moyo wa kila mtu kuwa ana jukumu kwa nduguye, anahisi kama anavyo hisi yeye, na anaungulika kama anavyo ungulika yeye. Kwa hivyo ni waajibu wake kufanya awezavyo kumkinga na balaa za kilimwengu, na machungu ya ukosefu. Kwa hivyo fakiri au masikini hatomchukia tajiri, bali wote watahisi kama ni ukoo mmoja unao saidiana na wenye kushikamana na Kamba ya Mwenyezi Mungu. Wala mwenye deni hakati tamaa kuweza kulipa deni lake lilio bakia ikiwa hana cha kumalizia hilo deni. Wala haianguki chini azma ya mujaahidi anaye pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuinusuru Dini yake na kukomboa nchi yake kwa sababu ya kukosa mali ya kutimizia makusudio yake. Wala msafiri au mgeni mhitaji aliye mbali na mali yake hakosi wa kumkidhia haja zake kwa kumsaidia mpaka afike kwake. Na juu ya haya Zaka ilikuwa ni njia moja katika njia kubwa ulio chukua Uislamu kukombolea mateka na wafungwa na kuondoa utumwa. Na Uislamu umeongeza kutimiza malengo yake ya kijamii kwa ulimwengu mzima ikatupilia mbali chuki zinazo chusha za kidini, na ikatoa ruhusa Zaka wapewe makafiri ikihitajia haja kuwakopesha. Hali kadhaalika hupewa wale wanao itumikia Zaka, kama kuikusanya na kuigawa. Pia waandishi, na wasafiri, na wanao khasiri kwa ajili ya kupatanisha wenye kugombana, na wanao wasaidia Waislamu katika vita. Ama makusudio ya kiuchumi ya Zaka ni kuondoa ufakiri popote ulipo, na kumsaidia kila mwenye haja kama ilivyo kwisha tangulia.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَٱلَّذِینَ هُمۡ لِفُرُوجِهِمۡ حَـٰفِظُونَ ﴿٥﴾

Na ambao wanazilinda tupu zao!

Nao wanajihifadhi nafsi zao wasiingiane na wanawake. "Na ambao wanazilinda tupu zao, isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa. Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka." Aya hizi zinaambatana na Aya nyengine ziliomo katika Suratun Nur zilio anzia: "Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mpigeni kila mmoja wao bakora mia." Hakika Aya hizi tukufu zilizo tajwa zinaashiria maovu ya katika umma yanayo tokea kwa uzinzi. Ama katika umma ni kuvurugika nasaba ya watoto isijuulikane, ama katika siha ni sehemu mbili. KWANZA ni katika mwili, mfano wa kisonono, tego, AIDS n.k. Kisonono huweza kuzalisha maradhi ya urithi kwa watoto hata huweza kuleta upofu. Ama tego (Syphilis) huenea katika mishipa ya damu na ya hisiya na huweza kuishia wazimu, na pia huenea mpaka kwa vizazi, na huenda mtoto akafa tumboni au akatoka na kilema. Ama maradhi ya AIDS (Ukimwi) hayo ni maafa yasiyo semeka, Mwenyezi Mungu atulinde nayo. PILI ni kuathirika mishipa ya hisiya na akili, kwani uzinzi huweza kuathiri dhamiri ya mtu, na kuadhibika nayo, na hata mwishoe huweza kuingia wazimu.


Arabic explanations of the Qur’an:

إِلَّا عَلَىٰۤ أَزۡوَ ٰ⁠جِهِمۡ أَوۡ مَا مَلَكَتۡ أَیۡمَـٰنُهُمۡ فَإِنَّهُمۡ غَیۡرُ مَلُومِینَ ﴿٦﴾

Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa.

Isipo kuwa kwa njia ya ndoa ya kisharia, au wenye kumiliki masuria. Hao hawalaumiwi. Zamani utumwa ulikuwa ni jambo la kawaida, na ilikuwa mtu akiweza kuchukua katika wajakazi wake akawafanya kuwa ni wakeze. Na Uislamu ulihalalisha utumwa wa mateka katika vita vilivyo fuata sharia ikiwa maadui nao wanakamata watumwa, basi ilikuwa ni halali kuwatendea wao hali kadhaalika. Ikiwa maadui hawawafanyi mateka kuwa ni watumwa basi ilikuwa haiwafalii Waislamu kuwafanya mateka kuwa ni watumwa.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَمَنِ ٱبۡتَغَىٰ وَرَاۤءَ ذَ ٰ⁠لِكَ فَأُوْلَـٰۤىِٕكَ هُمُ ٱلۡعَادُونَ ﴿٧﴾

Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka.

Mwenye kutaka kuingiliana na mwanamke bila ya kupitia njia hizi mbili, basi huyo amevuka mipaka ya sharia hadi ya kuvuka. Na (hao Waumini) wawe ni wenye kuhifadhi kila walicho pewa kuwa ni amana, ikiwa mali au neno au kitendo au chenginecho, na watimize kila ahadi iliyo baina yao na Mwenyezi Mungu au na watu. Wasikhuni amana, wala wasivunje ahadi.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَٱلَّذِینَ هُمۡ لِأَمَـٰنَـٰتِهِمۡ وَعَهۡدِهِمۡ رَ ٰ⁠عُونَ ﴿٨﴾

Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao!

Na (hao Waumini) wawe ni wenye kuhifadhi kila walicho pewa kuwa ni amana, ikiwa mali au neno au kitendo au chenginecho, na watimize kila ahadi iliyo baina yao na Mwenyezi Mungu au na watu. Wasikhuni amana, wala wasivunje ahadi.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَٱلَّذِینَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَوَ ٰ⁠تِهِمۡ یُحَافِظُونَ ﴿٩﴾

Na ambao Swala zao wanazihifadhi .

Na wawe wenye kudumisha kutimiza Swala kwa nyakati zake, na kuzitekeleza kwa nguzo zake na unyenyekevu wake, mpaka yapatikane makusudio yake. Nayo ni kuachisha uchafu na maovu.


Arabic explanations of the Qur’an:

أُوْلَـٰۤىِٕكَ هُمُ ٱلۡوَ ٰ⁠رِثُونَ ﴿١٠﴾

Hao ndio warithi,

Hawa wenye kusifiwa hivi ndio watakao rithi kheri yote na wataipata Siku ya Kiyama. Hawa ndio Mwenyezi Mungu atawafadhili kwa kuwapa Firdausi, ndio pahala pa juu kabisa huko Peponi, wastarehe humo peke yao.


Arabic explanations of the Qur’an:

ٱلَّذِینَ یَرِثُونَ ٱلۡفِرۡدَوۡسَ هُمۡ فِیهَا خَـٰلِدُونَ ﴿١١﴾

Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo.

Hawa ndio Mwenyezi Mungu atawafadhili kwa kuwapa Firdausi, ndio pahala pa juu kabisa huko Peponi, wastarehe humo peke yao.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن سُلَـٰلَةࣲ مِّن طِینࣲ ﴿١٢﴾

Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo.

Yawapasa watu waangalie asli ya kuumbwa kwao; kwani hiyo ni dalili za kuonyesha uwezo wetu zenye kupelekea kumuamini Mwenyezi Mungu, na kuamini kufufuliwa. Kwani Sisi tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo.


Arabic explanations of the Qur’an:

ثُمَّ جَعَلۡنَـٰهُ نُطۡفَةࣰ فِی قَرَارࣲ مَّكِینࣲ ﴿١٣﴾

Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti.

Kisha tukaumba vizazi vyake, navyo ni kuwa tulimfanya mtu kwanza tone ya mbegu ya uzazi - yaani maji yenye kila sifa ya uhai wa mwanzo. Tukaiweka kwenye tumbo la uzazi, napo ni pahala pa utulivu palipo lindwa.


Arabic explanations of the Qur’an:

ثُمَّ خَلَقۡنَا ٱلنُّطۡفَةَ عَلَقَةࣰ فَخَلَقۡنَا ٱلۡعَلَقَةَ مُضۡغَةࣰ فَخَلَقۡنَا ٱلۡمُضۡغَةَ عِظَـٰمࣰا فَكَسَوۡنَا ٱلۡعِظَـٰمَ لَحۡمࣰا ثُمَّ أَنشَأۡنَـٰهُ خَلۡقًا ءَاخَرَۚ فَتَبَارَكَ ٱللَّهُ أَحۡسَنُ ٱلۡخَـٰلِقِینَ ﴿١٤﴾

Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.

Kisha tukaifanya hii mbegu ya manii baada ya kuipandisha na yai la mwanamke kuwa damu. Kisha damu tukaigeuza kuwa kipande cha nyama, kisha tukafanya mafupa, na mafupa tukayavika nyama. Kisha tukatimiza uumbaji wake mwishoe baada ya kuipulizia roho kuwa kiumbe kingine mbali ili kuanza kumjenga. Shani ya Mwenyezi Mungu imetukuka kwa utukufu wake na uwezo wake. Yeye hana mshabaha wake na yeyote katika kuumba kwake na kutengeza kwake na kuanzisha kwake. Kisha hakika nyinyi wanaadamu baada ya haya mambo yenu tuliyo yataja ni wenye kuyaendea mauti bila ya shaka yoyote.


Arabic explanations of the Qur’an:

ثُمَّ إِنَّكُم بَعۡدَ ذَ ٰ⁠لِكَ لَمَیِّتُونَ ﴿١٥﴾

Kisha hakika nyinyi baada ya hayo mtakufa.

Kisha hakika nyinyi wanaadamu baada ya haya mambo yenu tuliyo yataja ni wenye kuyaendea mauti bila ya shaka yoyote.


Arabic explanations of the Qur’an:

ثُمَّ إِنَّكُمۡ یَوۡمَ ٱلۡقِیَـٰمَةِ تُبۡعَثُونَ ﴿١٦﴾

Kisha hakika nyinyi Siku ya Kiyama mtafufuliwa.

Na kisha nyinyi mtafufuliwa Siku ya Kiyama kwa ajili ya kuhisabiwa na kulipwa jaza yenu.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعَ طَرَاۤىِٕقَ وَمَا كُنَّا عَنِ ٱلۡخَلۡقِ غَـٰفِلِینَ ﴿١٧﴾

Na kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe.

Na hakika Sisi tumeziumba mbingu saba zilizo nyanyuka juu yenu. Ndani yake vipo viumbe ambavyo hatukughafilika navyo. Tunavihifadhi na tunaviendesha. Na Sisi kabisa hatughafiliki na viumbe vyetu vyote. Bali tunavilinda visipotee na kuharibika, na tunavipangia mambo yao yote kwa hikima. "Na kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe." Hizo njia saba zilizo tajwa katika hiyo Aya maana yake ni mbingu saba, na kwamba hizo si mbingu moja, na Mwenyezi Mungu haghafiliki na mbingu hizo na viumbe viliomo ndani yake.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَاۤءِ مَاۤءَۢ بِقَدَرࣲ فَأَسۡكَنَّـٰهُ فِی ٱلۡأَرۡضِۖ وَإِنَّا عَلَىٰ ذَهَابِۭ بِهِۦ لَقَـٰدِرُونَ ﴿١٨﴾

Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na tukayatuliza katika ardhi. Na hakika Sisi tunaweza kuyaondoa.

Na Sisi tumeteremsha kutoka mbinguni mvua kwa hikima na kipimo katika umbo lake na kuteremka kwake. Na kusahilisha kwa ajili ya manufaa tumeijaalia ikae juu ya uso wa ardhi na ndani yake chini. Na Sisi hakika ni wenye kuweza kuiondoa wasipate kunafiika nayo. Lakini hatukufanya hayo kwa kukuoneeni huruma. Basi muaminini Mwenye kuiumba na mumshukuru. "Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na tukayatuliza katika ardhi. Na hakika Sisi tunaweza kuyaondoa." Aya hii tukufu inaashiria maana ya kisayansi yenye kukhusu mzunguko wa maji katika ardhi. Yajuulikana kuwa mvuke unao paa kutoka baharini hupelekea kufanyika mawingu ambayo ndiyo huteremsha mvua. Na hivyo ndio chanzo cha maji matamu juu ya uso wa ardhi, na ndio chombo cha msingi cha uhai wa ardhini. Kutokana na mvua ndio huzuka mito inayo zua uhai katika sehemu kamwe zisio pitikiwa na mvua. Kisha hiyo mito inamiminika baharini, na khulka inarejea tena kutoka baharini kwenda angani na kwendea nchi kavu, na kisha kuingia baharini mara ya pili. Isipo kuwa baadhi ya hayo maji ya mvua yanatulia na yanazama kuhifadhika katika mahodhi ya chini ya ardhi, yakawekeka kwa muda mrefu. Mfano wa hayo ni hayo maji yanayo patikana chini ya Jangwa la Magharibi katika Libya, ambayo yamegunduliwa na watafiti hivi karibuni kutokana na asli yake ya kale. Na huenda maji kama haya yalio hifadhika chini yakapatwa na mabadiliko ya joto wanayo yaita wataalamu wa ilimu ya t'abaka za ardhi (Geology) kuwa ni Mikondo ya Jiolojia, ikenda hiyo na maji mpaka pahala pengine pakavu, ikaleta uhai baada ya kuwa ni maiti. Na Aya hii inaonyesha hikima kubwa ya uenezaji wa maji kwa kipimo, yaani kipimo cha haki na hikima, kwa ajili ya kuleta manufaa na kupinga madhara. Na tena maana nyengine ya Aya tukufu ni kufahamisha apendavyo Mwenye Kuumba, Aliye tukuka, navyo ni kujaalia yawepo maji ya kiasi maalumu katika bahari za ulimwengu kutosha kuwepo mizani ya joto la kufaa katika sayari hii, na ili isiwepo khitilafu kubwa mno baina ya joto la siku za joto, na baridi ya siku za baridi, hata ikawa ni muhali kubakia uhai, kama ilivyo katika sayari nyengine na katika mwezi. Kadhaalika maji ya ardhi yanateremka kwa kiasi maalumu, hayazidi yakafunika ardhi yote, wala hayatindikii sana hata yasipatikane hata kidogo kunyweshea baadhi ya nchi kavu.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَأَنشَأۡنَا لَكُم بِهِۦ جَنَّـٰتࣲ مِّن نَّخِیلࣲ وَأَعۡنَـٰبࣲ لَّكُمۡ فِیهَا فَوَ ٰ⁠كِهُ كَثِیرَةࣱ وَمِنۡهَا تَأۡكُلُونَ ﴿١٩﴾

Kwa maji hayo tukakufanyieni bustani za mitende na mizabibu, mnapata humo matunda mengi, na katika hayo mnakula;

Kwa haya maji tukakuumbieni mabustani ya mitende na mizabibu yenye matunda mengi kwa ajili yenu, na katika hayo nyinyi mnakula.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَشَجَرَةࣰ تَخۡرُجُ مِن طُورِ سَیۡنَاۤءَ تَنۢبُتُ بِٱلدُّهۡنِ وَصِبۡغࣲ لِّلۡـَٔاكِلِینَ ﴿٢٠﴾

Na mti utokao katika mlima wa Sinai, unatoa mafuta na kuwa kitoweo kwa walao.

Na tumekuumbieni mti wa zaituni unao ota katika jimbo la Mlima wa Sinai. Katika matunda yake yanapatikana mafuta yanayo kufaeni. Na hizo zaituni ni kitoweo cha chakula kwa wanao kula. "Na mti utokao katika mlima wa Sinai, unatoa mafuta na kuwa kitoweo kwa walao." Aya hii tukufu inathibitisha kuwa mti wa zaituni ni miongoni mwa neema alizo mneemesha Mwenyezi Mungu binaadamu na ambazo baadhi yake zimetajwa katika Aya zilizo tangulia. Na la kuongeza kwenye Aya hii ni kuwa mzaituni ni miongoni mwa miti ya mbao inayo ishi muda mrefu sana, zaidi ya mamia ya miaka. Kwa hivyo hauhitajii juhudi kubwa kwa mtu, bali huendelea kuzaa wenyewe mfululizo. Kadhaalika una sifa ya kuwa daima kijani, unapendeza kuutazama. Uchunguzi wa kisayansi unaonyesha kwamba zaituni ni katika chakula kizuri. Kwani ndani yake imo Protein nyingi. Vile vile zimo chumvi za Calcium, chuma na Phospohorous. Na hivi ni muhimu na vya kutegemewa katika chakula cha binaadamu. Na juu ya hivyo zaituni inayo Vitamin A na Vitamin B. Na kutokana na tunda lake hutolewa mafuta ya zaituni, ambayo ni mafuta bora ya mafuta mepesi. Mafuta haya hutumiwa katika chakula. Uchunguzi wa kitabibu unaongeza kusema kuwa zipo faida nyengine katika mafuta ya zaituni, nazo ni kuwa zinasaidia kwa jumla katika viungo vya usagaji wa chakula, na khasa maini. Nayo yanashinda ubora mafuta yote yanayo tokana na mimea na wanyama, kwa kuwa hayasabibishi maradhi ya mishipa ya damu kama mafuta mengineyo, na kadhaalika yanalainisha ngozi. Na mafuta ya zaituni yana matumizi mengine mengi katika sanaa (ufundi), kwani yanatumiwa katika kufanya sabuni nzuri kabisa, na vitu vinginevyo katika ufanyaji wa vyakula na vitu vya sanaa.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَإِنَّ لَكُمۡ فِی ٱلۡأَنۡعَـٰمِ لَعِبۡرَةࣰۖ نُّسۡقِیكُم مِّمَّا فِی بُطُونِهَا وَلَكُمۡ فِیهَا مَنَـٰفِعُ كَثِیرَةࣱ وَمِنۡهَا تَأۡكُلُونَ ﴿٢١﴾

Na hakika mnayo mazingatio makubwa katika nyama hoa - tunakunywesheni katika vile viliomo matumboni mwao, na nyinyi mnapata katika hao manufaa mengi, na pia mnawala.

Na nyinyi mnapata kutokana na nyama hoa, nyama wa kufuga, nao ni ngamia, ng'ombe, kondoo na mbuzi, mambo yanayo onyesha uwezo wetu na fadhila zetu juu yenu kwa kukuneemesheni. Tunakunywesheni kutoka matumboni mwao maziwa safi, matamu, mepesi kwa wenye kuyanywa. Na mbali ya maziwa mnapata manufaa mengine kama nyama, na sufi, na manyoya. Na kutokana na hao nyinyi mnaishi na mnaruzukiwa.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَعَلَیۡهَا وَعَلَى ٱلۡفُلۡكِ تُحۡمَلُونَ ﴿٢٢﴾

Na juu yao na juu ya marikebu mnabebwa.

Na juu ya hawa wanyama wa kufuga na marikebu nyinyi mnapanda, na mnapakia mizigo. Basi Sisi tumekuumbieni njia za usafirishaji na upakizi nchi kavu na baharini. Na kwa hizo mnapata kuwasiliana nyinyi kwa nyinyi.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ فَقَالَ یَـٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَـٰهٍ غَیۡرُهُۥۤۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٢٣﴾

Na hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu asiye kuwa Yeye. Basi je! Hamwogopi?

Na katika visa vya watu wa kale pana mazingatio kwa ajili yenu mpate kuamini. Basi Sisi tulimtuma Nuhu kwa watu wake, naye akawaambia: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu pekee. Kwani nyinyi hamna anaye stahiki kuabudiwa asiye kuwa Yeye. Hamwogopi adhabu yake, na kuondoka neema zake mkimuasi?


Arabic explanations of the Qur’an:

فَقَالَ ٱلۡمَلَؤُاْ ٱلَّذِینَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ مَا هَـٰذَاۤ إِلَّا بَشَرࣱ مِّثۡلُكُمۡ یُرِیدُ أَن یَتَفَضَّلَ عَلَیۡكُمۡ وَلَوۡ شَاۤءَ ٱللَّهُ لَأَنزَلَ مَلَـٰۤىِٕكَةࣰ مَّا سَمِعۡنَا بِهَـٰذَا فِیۤ ءَابَاۤىِٕنَا ٱلۡأَوَّلِینَ ﴿٢٤﴾

Walisema wale wakuu walio kufuru katika watu wake: Huyu si chochote ila ni mtu tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu amependa basi yakini angeli teremsha Malaika. Hatukusikia haya kwa baba zetu wa zamani.

Wakubwa wa kaumu yake walio kufuru wakiukanya wito wake na wakizuia watu wasimfuate, walisema: Hapana khitilafu yoyote baina ya Nuhu na nyinyi. Kwani yeye ni mtu kama nyinyi, lakini anataka kujipa ubora juu yenu kwa huu wito wake. Na lau kuwa wapo Mitume wanao toka kwa Mwenyezi Mungu kama anavyo dai yeye, basi ange waletea Malaika. Sisi hatukupata kusikia wito huu katika taarikhi za baba zetu walio tangulia, wala kutumwa binaadamu kuwa ni Mtume.


Arabic explanations of the Qur’an:

إِنۡ هُوَ إِلَّا رَجُلُۢ بِهِۦ جِنَّةࣱ فَتَرَبَّصُواْ بِهِۦ حَتَّىٰ حِینࣲ ﴿٢٥﴾

Huyu si lolote ila ni mtu mwenye wazimu. Basi mngojeeni tu kwa muda.

Huyu si chochote ila ni mtu mwenye wazimu. Na kwa hivyo wakasema: Ngojeni, na mstahamilieni mpaka ukashifike wazimu wake, au kufike kuangamia kwake.


Arabic explanations of the Qur’an:

قَالَ رَبِّ ٱنصُرۡنِی بِمَا كَذَّبُونِ ﴿٢٦﴾

Akasema (Nuhu): Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa kuwa wamenikanusha.

Nuhu akamwomba Mola wake Mlezi baada ya kukata tamaa kuamini kwao, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ninusuru nao, na watie adabu kwa sababu ya kuukadhibisha kwao wito wangu!


Arabic explanations of the Qur’an:

فَأَوۡحَیۡنَاۤ إِلَیۡهِ أَنِ ٱصۡنَعِ ٱلۡفُلۡكَ بِأَعۡیُنِنَا وَوَحۡیِنَا فَإِذَا جَاۤءَ أَمۡرُنَا وَفَارَ ٱلتَّنُّورُ فَٱسۡلُكۡ فِیهَا مِن كُلࣲّ زَوۡجَیۡنِ ٱثۡنَیۡنِ وَأَهۡلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَیۡهِ ٱلۡقَوۡلُ مِنۡهُمۡۖ وَلَا تُخَـٰطِبۡنِی فِی ٱلَّذِینَ ظَلَمُوۤاْ إِنَّهُم مُّغۡرَقُونَ ﴿٢٧﴾

Tukampa wahyi: Unda jahazi mbele ya macho yetu na uwongozi wetu! Basi itapo fika amri yetu na ikafurika tanuri, hapo waingize ndani yake wa kila namna dume na jike, na ahali zako, isipo kuwa yule ambaye katika wao juu yake imekwisha tangulia kauli. Wala usinitajie hao walio dhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa.

Tukamwambia kwa njia ya ufunuo (wahyi): Unda jahazi, nawe utalindwa na uangalizi wetu. Shari yao haitokupata, nasi tutakuongoza katika kazi yako. Na ikifikilia miadi ya kuwaadhibu, na ukaona tanuri inafoka maji kwa amri yetu, basi waingize katika jahazi katika kila namna ya viumbe vilivyo hai dume na jike. Na waingize ahali zako, isipo kuwa walio kwisha thibitika adhabu yao kwa kukosa kwao Imani. Wala usiniombe kuwaokoa wale walio dhulumu nafsi zao na wakawadhulumu na wengineo kwa ukafiri na uasi. Kwani Mimi nimewahukumia kuwazamisha kwa sababu ya dhulma yao ya ushirikina na uasi. "Tukampa wahyi: Unda jahazi mbele ya macho yetu na uwongozi wetu! Basi itapo fika amri yetu na ikafurika tanuri, hapo waingize ndani yake wa kila namna dume na jike, na ahali zako, isipo kuwa yule ambaye katika wao juu yake imekwisha tangulia kauli. Wala usinitajie hao walio dhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa." Hakika haya maelezo ya Tofani lilio tokea ijapo kuwa ni kwa mukhtasari tu katika hizi Aya tukufu, kwa mwenye akili ya kuzingatia yana maana na mambo ya hakika mengi ya ki-ilimu ambayo yanawapitia watu wengi. Na "tanuri" kwa lugha ni jiko la kuchomea mikate, au pia ni uso wa ardhi na kila chenye kutimbuka maji, na kila penye mkusanyiko wa maji. Na si wepesi kusema kwa yakini taarikhi ya hiyo Tofani, kwani zilitokea tofani nyingi zama za kale, kama katika Babilonia, Bara Hindi na Amerika. Na zipo baadhi ya hadithi za kienyeji mbali mbali zinazo taja khabari ya Tofani. Lakini haielekei kuwa hadithi hizo ndio zimekhusu hii Tofani kubwa au Tofani ya Nuhu. Uchunguzi umethibitisha na pia zimeonekana tofani nyingi ulimwenguni. Na tofani ya mwisho ya ulimwengu mzima ilikuwa sababu yake ni kumalizika kipindi cha barafu cha mwisho, na kuyayuka barafu nyingi ya kaskazini kabisa na kusini kabisa kwa dunia. Na sisi hatujui kwa yakini lini mizani iligeuka na tanuri ikafurika - yaani uso wa ardhi - kwa kupanda kwa ghafla kwa hivyo kuyayuka barafu, hata yakapanda juu maji ya bahari na ya kamwagika maji. Yafaa kutaja kuwa kuyayuka barafu ya zama za barafu za mwisho kulileta hali ya hewa yenye mvua nyingi sana katika sehemu za dunia zilio mbali na huko kaskazini na kusini kabisa kwa ulimwengu, kama vile katika Bahari ya Kati (Mediterenian). Vyo vyote vile ilivyo inakubalika kuwa hatuna ushahidi wa kuweza kusema lini khasa zilikuwa hizo zama za Nuhu na kaumu yake. Yaliyo dhaahiri kuwa yote hayo ni muujiza wa Mwenyezi Mungu. Na katika miujiza ni kuwa Nuhu aliwanasihi watu wake na akawaonya na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu akafunua kuwa atawazamisha ikiwa hawakutengenea. Na tena akamfunulia aunde marikebu. Kisha ikaja amri ya Mwenyezi Mungu, na mizani ikapinduka, na tanuri ikafurika, ikamiminika mvua kuthibitisha aliyo yasema Mwenyezi Mungu kumwambia Nuhu ya kwamba Mwenyezi Mungu anajua kuwa hatoamini mtu katika kaumu yake baada ya wale walio kwisha amini.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَإِذَا ٱسۡتَوَیۡتَ أَنتَ وَمَن مَّعَكَ عَلَى ٱلۡفُلۡكِ فَقُلِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِی نَجَّىٰنَا مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّـٰلِمِینَ ﴿٢٨﴾

Basi utakapo tulia wewe na walio pamoja nawe humo marikebuni, sema: Alhamdulillahi Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, aliye tuokoa na watu madhaalimu!

Na ukisha panda na ukatua wewe na walio pamoja nawe katika jahazi hiyo basi sema kwa kumshukuru Mola wako Mlezi: Alhamdulillahi! Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliye tuokoa na shari ya watu makafiri walio asi.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَقُل رَّبِّ أَنزِلۡنِی مُنزَلࣰا مُّبَارَكࣰا وَأَنتَ خَیۡرُ ٱلۡمُنزِلِینَ ﴿٢٩﴾

Na sema: Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ni Mbora wa wateremshaji.

Na useme: Ewe Mola Mlezi! Nijaalie nishuke mashukio yenye baraka, pahala pazuri pa kukaa wakati wa kuteremka nchi kavu. Na unitunukie amani hapo. Kwani ni Wewe tu peke yako unaye weza kututeremsha pahala pa kheri na amani na salama.


Arabic explanations of the Qur’an:

إِنَّ فِی ذَ ٰ⁠لِكَ لَـَٔایَـٰتࣲ وَإِن كُنَّا لَمُبۡتَلِینَ ﴿٣٠﴾

Hakika katika hayo yapo mazingatio. Na kwa yakini Sisi ni wenye kuwafanyia mtihani.

Hakika katika kisa hichi yapo mazingatio na mawaidha mengi. Na hakika Sisi tunawajaribu (tunawapa mitihani) waja wetu kwa kheri na shari. Na ndani ya nafsi zao wana utayarisho wa yote hayo.


Arabic explanations of the Qur’an:

ثُمَّ أَنشَأۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِمۡ قَرۡنًا ءَاخَرِینَ ﴿٣١﴾

Kisha baada yao, tukanzisha kizazi kingine.

Tena baada ya kaumu ya Nuhu tukaumba namna ya watu wengine, na wao ni A'adi.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَأَرۡسَلۡنَا فِیهِمۡ رَسُولࣰا مِّنۡهُمۡ أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَـٰهٍ غَیۡرُهُۥۤۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٣٢﴾

Tukawapelekea Mtume miongoni mwao, kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu asiye kuwa Yeye. Jee, hamwogopi?

Tukawapelekea Huud. Naye ni katika wao. Tukawaambia kwa ulimi wake: Muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake. Kwani nyinyi hamna Mungu anaye stahiki kuabudiwa asiye kuwa Yeye. Ni Yeye peke yake anaye faa mumwogope. Basi, jee mmeikhofu adhabu yake mkimuasi?


Arabic explanations of the Qur’an:

وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِهِ ٱلَّذِینَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِلِقَاۤءِ ٱلۡـَٔاخِرَةِ وَأَتۡرَفۡنَـٰهُمۡ فِی ٱلۡحَیَوٰةِ ٱلدُّنۡیَا مَا هَـٰذَاۤ إِلَّا بَشَرࣱ مِّثۡلُكُمۡ یَأۡكُلُ مِمَّا تَأۡكُلُونَ مِنۡهُ وَیَشۡرَبُ مِمَّا تَشۡرَبُونَ ﴿٣٣﴾

Na wakubwa katika watu wake walioukufuru, na wakakanusha mkutano wa Akhera, na tukawadekeza kwa starehe, katika maisha ya dunia, walisem: Huyu si chochote ila ni mwanadamu kama nyinyi, anakula mlacho, na anakunywa mnywacho.

Na wakubwa katika kaumu yake walio kufuru na kukadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu na mambo ya Akheria ya hisabu na malipo, na tukawapa sehemu kubwa ya starehe na neema, wakasema kwa kukanusha wito wake, na kuwazuia watu wasimfuate: Hapana khitilafu yo yote baina ya Huud na nyinyi. Anakula chakula hicho hicho mnacho kila nyinyi. Na anakunywa vinywaji hivyo hivyo mnavyo vinywa nyinyi. Mfano wa huyu hawezi kuwa Mtume, kwa sababu hana sifa msizo kuwa nazo nyinyi.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَلَىِٕنۡ أَطَعۡتُم بَشَرࣰا مِّثۡلَكُمۡ إِنَّكُمۡ إِذࣰا لَّخَـٰسِرُونَ ﴿٣٤﴾

Na nyinyi mkimt'ii mtu kama nyinyi basi hakika mtakuwa khasarani.

Na wakawahadharisha kwa nguvu na mkazo, wakiwaambia: Mkimt'ii mtu aliye kama nyinyi kwa utu wake, basi nyinyi hakika mtakuwa mmekhasiri kwa kuwa hamtapata manufaa yo yote mkimfuata.


Arabic explanations of the Qur’an:

أَیَعِدُكُمۡ أَنَّكُمۡ إِذَا مِتُّمۡ وَكُنتُمۡ تُرَابࣰا وَعِظَـٰمًا أَنَّكُم مُّخۡرَجُونَ ﴿٣٥﴾

Hivyo anakuahidini ati ya kwamba mtakapo kufa na mkawa udongo na mifupa kuwa mtatolewa?

Wakawaambia pia katika kukanya kufufuliwa: Hivyo Huud anakuahidini kuwa mtafufuliwa kutoka makaburini kwenu baada ya kwisha kufa kwenu, na mkawa udongo na mafupa yasiyo kuwa na nyama na mishipa?


Arabic explanations of the Qur’an:

۞ هَیۡهَاتَ هَیۡهَاتَ لِمَا تُوعَدُونَ ﴿٣٦﴾

Hayawi! Hayawi hayo mnayo ahidiwa.

Hayo anayo kuahidini ni ya mbali mno, wala hayatakuwa abadan.


Arabic explanations of the Qur’an:

إِنۡ هِیَ إِلَّا حَیَاتُنَا ٱلدُّنۡیَا نَمُوتُ وَنَحۡیَا وَمَا نَحۡنُ بِمَبۡعُوثِینَ ﴿٣٧﴾

Hapana ila uhai wetu wa duniani tu, tunakufa na kuishi basi. Wala sisi hatutafufuliwa.

Hapana uhai ila mmoja tu. Nao ndio huu uhai wa duniani, ambao tunauona una mauti na uhai unao tupitia. Kinacho zaliwa kinazaliwa, na kilicho hai kinakufa. Wala hatutofufuliwa baada ya kwisha kufa kabisa.


Arabic explanations of the Qur’an:

إِنۡ هُوَ إِلَّا رَجُلٌ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبࣰا وَمَا نَحۡنُ لَهُۥ بِمُؤۡمِنِینَ ﴿٣٨﴾

Huyu si lolote ila ni mtu anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, wala sisi sio wa kumuamini.

Huyu si chochote ila ni mtu aliye mzulia Mwenyezi Mungu, na akadai kwamba Mwenyezi Mungu kamtuma yeye. Na amesema uwongo katika hayo anayo tuitia. Wala hatutomsadiki abadan. *


Arabic explanations of the Qur’an:

قَالَ رَبِّ ٱنصُرۡنِی بِمَا كَذَّبُونِ ﴿٣٩﴾

Akasema: Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa sababu wananikanusha.

Huud akasema baada ya kwisha kata tamaa kuamini kwao: Ewe Mola wangu Mlezi! Ninusuru na uwatie adabu, kwa sababu ya kuukadhibisha wito wangu.


Arabic explanations of the Qur’an:

قَالَ عَمَّا قَلِیلࣲ لَّیُصۡبِحُنَّ نَـٰدِمِینَ ﴿٤٠﴾

(Mwenyezi Mungu) akasema: Baada ya muda mchache watakuwa wenye kujuta.

Mwenyezi Mungu akamwambia Huud kuzidi kutilia nguvu ahadi yake: Baada ya muda mchache watakuja juta, kwa waliyo yafanya, itapo wateremkia adhabu.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّیۡحَةُ بِٱلۡحَقِّ فَجَعَلۡنَـٰهُمۡ غُثَاۤءࣰۚ فَبُعۡدࣰا لِّلۡقَوۡمِ ٱلظَّـٰلِمِینَ ﴿٤١﴾

Basi ukawanyakua ukelele kwa haki, na tukawafanya kama takataka zinazo elea juu ya maji. Ikapotelea mbali kaumu ya madhaalimu!

Ukawachukua ukelele mkali ulio wahilikisha kama walivyo stahiki. Tukawafanya kwa udhalili na udhaifu kama vijiti na majani ya miti yanayo chukuliwa na maji ya mvua. Na huko ni kuteketea na kupotelea mbali na rehema kwa madhaalimu kwa ukafiri wao na uasi wao.


Arabic explanations of the Qur’an:

ثُمَّ أَنشَأۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِمۡ قُرُونًا ءَاخَرِینَ ﴿٤٢﴾

Kisha tukaleta baada yao vizazi vingine.

Kisha baada yao tukawaumba kaumu nyengine wasio kuwa wao, kama kaumu ya Swaleh na ya Luut'i na ya Shuaib.


Arabic explanations of the Qur’an:

مَا تَسۡبِقُ مِنۡ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا یَسۡتَـٔۡخِرُونَ ﴿٤٣﴾

Hapana umma uwezao kutanguliza ajali yake wala kuikawiza.

Kila umma una zama zake maalumu, hazitangulii wala hazikawii.


Arabic explanations of the Qur’an:

ثُمَّ أَرۡسَلۡنَا رُسُلَنَا تَتۡرَاۖ كُلَّ مَا جَاۤءَ أُمَّةࣰ رَّسُولُهَا كَذَّبُوهُۖ فَأَتۡبَعۡنَا بَعۡضَهُم بَعۡضࣰا وَجَعَلۡنَـٰهُمۡ أَحَادِیثَۚ فَبُعۡدࣰا لِّقَوۡمࣲ لَّا یُؤۡمِنُونَ ﴿٤٤﴾

Kisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipo wafikia Mtume wao walimkanusha. Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa, na tukawafanya ni hadithi za kusimuliwa. Wakapotelea mbali watu wasio amini.

Kisha tukawatuma Mitume wetu wakifuatana, kila mmoja kwa kaumu yake. Kila akija Mtume kwa kaumu yake waliukadhibisha wito wake. Nasi tukawateketeza mfululizo, na tukazifanya khabari zao ni hadithi za watu kusimuliana na kuzistaajabia. Basi hao kaumu wasio isadiki Haki wala hawaifuati wametengeka mbali na rehema, na wamehiliki.


Arabic explanations of the Qur’an:

ثُمَّ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ وَأَخَاهُ هَـٰرُونَ بِـَٔایَـٰتِنَا وَسُلۡطَـٰنࣲ مُّبِینٍ ﴿٤٥﴾

Kisha tukamtuma Musa na nduguye, Haaruni, pamoja na ishara zetu na hoja zilizo wazi.

Kisha tukamtuma Musa na nduguye, Haaruni, tukawapa dalili za kukata kuthibitisha ukweli wa ujumbe wao, na hoja wazi yenye kudhihirisha kuwa wao ni kweli wametumwa kutoka kwangu.


Arabic explanations of the Qur’an:

إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِیْهِۦ فَٱسۡتَكۡبَرُواْ وَكَانُواْ قَوۡمًا عَالِینَ ﴿٤٦﴾

Kumwendea Firauni na wakuu wake. Lakini walijivuna, nao walikuwa watu majeuri.

Tuliwatuma wawili hao kwa Firauni na kaumu yake. Wakakataa kuamini kwa ajili ya takaburi, na wao ni watu walio kuwa wakisifika kwa kiburi, na majivuno, na ujeuri.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَقَالُوۤاْ أَنُؤۡمِنُ لِبَشَرَیۡنِ مِثۡلِنَا وَقَوۡمُهُمَا لَنَا عَـٰبِدُونَ ﴿٤٧﴾

Wakasema: Je, tuwaamini wanaadamu wawili hawa kama sisi, na ambao watu wao ni watumwa wetu?

Wakasema kwa mastaajabu na kukanya: Je, tuuamini wito wa watu wawili walio ni wanaadamu kama sisi, na tena watu wao hawa Wana wa Israili ni wenye kutunyenyekea sisi na kutut'ii kama ni watumwa?


Arabic explanations of the Qur’an:

فَكَذَّبُوهُمَا فَكَانُواْ مِنَ ٱلۡمُهۡلَكِینَ ﴿٤٨﴾

Basi wakawakanusha, na wakawa miongoni mwa walio angamizwa.

Basi waliwafanya waongo katika huo wito wao, na wakawa wenye kuhiliki kwa kuzamishwa.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَلَقَدۡ ءَاتَیۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَـٰبَ لَعَلَّهُمۡ یَهۡتَدُونَ ﴿٤٩﴾

Na hakika tulimpa Musa Kitabu ili wapate kuongoka.

Na hakika tulimfunulia Musa Taurati apate kuwaongoa watu wake kwa yaliyomo ndani yake ya uwongozi kwendea hukumu na njia za mafanikio.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَجَعَلۡنَا ٱبۡنَ مَرۡیَمَ وَأُمَّهُۥۤ ءَایَةࣰ وَءَاوَیۡنَـٰهُمَاۤ إِلَىٰ رَبۡوَةࣲ ذَاتِ قَرَارࣲ وَمَعِینࣲ ﴿٥٠﴾

Na tukamfanya mwana wa Mariamu na mama yake kuwa ni Ishara, na tukawapa makimbilio kwenda mahali palipo inuka penye utulivu na chemchem za maji.

Na tumemjaalia Isa bin Maryamu na mama yake, kwa vile kuchukua mimba bila ya kuingiliwa na mtu, na kuzaliwa yeye Isa bila ya baba, kuwa dalili ya kukata ya uwezo wetu wenye kushinda. Na tukamweka Maryamu pahala pa kukaa penye ardhi iliyo nyanyuka na kukunjuka panapo faa kukaa, na pana maji mengi. Na hayo ndiyo yanayo wezesha maisha ya starehe.


Arabic explanations of the Qur’an:

یَـٰۤأَیُّهَا ٱلرُّسُلُ كُلُواْ مِنَ ٱلطَّیِّبَـٰتِ وَٱعۡمَلُواْ صَـٰلِحًاۖ إِنِّی بِمَا تَعۡمَلُونَ عَلِیمࣱ ﴿٥١﴾

Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa mnayo yatenda.

Tumewaambia Mitume wawafikishie watu wao: Kuleni vyakula vya kila namna vya halali na vizuri, na stareheni na ishukuruni neema yangu kwa vitendo vyema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa myatendayo na nitakulipeni kwayo.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَإِنَّ هَـٰذِهِۦۤ أُمَّتُكُمۡ أُمَّةࣰ وَ ٰ⁠حِدَةࣰ وَأَنَا۠ رَبُّكُمۡ فَٱتَّقُونِ ﴿٥٢﴾

Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi.

Na tukawaambia wawafikishie watu wao: Hakika hii Dini niliyo kutumeni muifikishe ni Dini moja kwa mintarafu ya Imani na misingi ya sharia. Na hakika nyinyi ni umma mmoja katika vizazi vyote. Miongoni mwao wapo walio ongoka, na wapo walio potoka. Na Mimi ndiye Mola wenu Mlezi niliye kuamrisheni muifuate, basi iogopeni adhabu yangu pindi mkiasi.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَتَقَطَّعُوۤاْ أَمۡرَهُم بَیۡنَهُمۡ زُبُرࣰاۖ كُلُّ حِزۡبِۭ بِمَا لَدَیۡهِمۡ فَرِحُونَ ﴿٥٣﴾

Lakini walikatiana jambo lao mapande mbali mbali. Kila kundi likifurahia kwa waliyo nayo.

Lakini watu walilikata kata hili jambo la Dini yao. Wapo kati yao walio ongoka, na wapo walio potoka ambao wakafuata matamanio yao, wakafarikiana kwa sababu hiyo wakawa makundi mbali mbali yenye kufanyiana uadui. Kila kikundi kinafurahi kwa walio nayo, kwa kudhania kuwa wao tu ndio walio sibu.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَذَرۡهُمۡ فِی غَمۡرَتِهِمۡ حَتَّىٰ حِینٍ ﴿٥٤﴾

Basi waache katika ghafla yao kwa muda.

Basi, ewe Muhammad, waachilie mbali makafiri na ujinga wao na kughafilika kwao, maadamu wewe umekwisha wanasihi, mpaka Mwenyezi Mungu awahukumie adhabu baadae.


Arabic explanations of the Qur’an:

أَیَحۡسَبُونَ أَنَّمَا نُمِدُّهُم بِهِۦ مِن مَّالࣲ وَبَنِینَ ﴿٥٥﴾

Je! Wanadhani ya kuwa kwa vile tunavyo wapa mali na watoto

Hivyo hawa maasi wanadhani ya kwamba pale Sisi tunapo wawacha wakistarehe na mali na watoto tulio wapa


Arabic explanations of the Qur’an:

نُسَارِعُ لَهُمۡ فِی ٱلۡخَیۡرَ ٰ⁠تِۚ بَل لَّا یَشۡعُرُونَ ﴿٥٦﴾

Ndio tunawahimizia kheri? Lakini wenyewe hawatambui.

Ndio basi Sisi tumekuwa radhi nao, na kheri zikawamiminikia mbio mbio na kwa wingi? Hao ni kama wanyama, hawatambui, kwa kuwa hawazitumii akili zao. Mimi si radhi nao. Na hizi neema ni kuwapururia tu, kuwapa muda.


Arabic explanations of the Qur’an:

إِنَّ ٱلَّذِینَ هُم مِّنۡ خَشۡیَةِ رَبِّهِم مُّشۡفِقُونَ ﴿٥٧﴾

Kwa hakika hao ambao kwa kumwogopa Mola wao Mlezi wananyenyekea,

Hakika wale ambao humkhofu Mwenyezi Mungu na humwogopa, na zimejaa ndani yao khofu ya Mwenyewe Subhanahu,


Arabic explanations of the Qur’an:

وَٱلَّذِینَ هُم بِـَٔایَـٰتِ رَبِّهِمۡ یُؤۡمِنُونَ ﴿٥٨﴾

Na wale ambao Ishara za Mola wao Mlezi wanaziamini,

Na wale ambao wanaziamini Ishara za Mola wao Mlezi ziliomo ulimwenguni na zinazo somwa katika Kitabu kilicho teremshwa,


Arabic explanations of the Qur’an:

وَٱلَّذِینَ هُم بِرَبِّهِمۡ لَا یُشۡرِكُونَ ﴿٥٩﴾

Na wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi,

Na wale ambao hawamshirikishi Mwenyezi Mungu na yeyote,


Arabic explanations of the Qur’an:

وَٱلَّذِینَ یُؤۡتُونَ مَاۤ ءَاتَواْ وَّقُلُوبُهُمۡ وَجِلَةٌ أَنَّهُمۡ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ رَ ٰ⁠جِعُونَ ﴿٦٠﴾

Na wale ambao wanatoa walicho pewa, na hali nyoyo zao zinagopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi,

Na wale ambao wanatoa katika vile anavyo waruzuku Mwenyezi Mungu, na wanafanya a'mali yao na hali wao wana khofu wasifanye taksiri, kwa sababu bila ya shaka wao ni wenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa kufufuliwa na watahisabiwa,


Arabic explanations of the Qur’an:

أُوْلَـٰۤىِٕكَ یُسَـٰرِعُونَ فِی ٱلۡخَیۡرَ ٰ⁠تِ وَهُمۡ لَهَا سَـٰبِقُونَ ﴿٦١﴾

Basi wote hao ndio wanao kimbilia katika mambo ya kheri, na ndio watakao tangulia kuyafikia.

Hao wote hukimbilia na a'mali zao kuendea kupata kheri, na wao ni wenye kuwatangulia wengineo katika kupata huko.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَلَا نُكَلِّفُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَاۚ وَلَدَیۡنَا كِتَـٰبࣱ یَنطِقُ بِٱلۡحَقِّ وَهُمۡ لَا یُظۡلَمُونَ ﴿٦٢﴾

Na hatuilazimishi nafsi ila kwa kadri ya uwezo wake. Na tunacho kitabu kisemacho kweli. Nao hawatadhulumiwa.

Na Sisi hatumlazimishi mtu yeyote ila kwa analo liweza kulifanya, kwa sababu limo ndani ya makdara yake. Na kila a'mali katika a'mali za waja zimesajiliwa kwetu katika kitabu, na tutawapa khabari zake kama zilivyo. Na wao hawatadhulumiwa kwa kuongezewa adhabu wala kupunguziwa thawabu.


Arabic explanations of the Qur’an:

بَلۡ قُلُوبُهُمۡ فِی غَمۡرَةࣲ مِّنۡ هَـٰذَا وَلَهُمۡ أَعۡمَـٰلࣱ مِّن دُونِ ذَ ٰ⁠لِكَ هُمۡ لَهَا عَـٰمِلُونَ ﴿٦٣﴾

Lakini nyoyo zao zimeghafilika na hayo, na wanavyo vitendo vinginevyo wanavyo vifanya.

Lakini makafiri kwa sababu ya inadi yao na chuki zao ni wenye kughafilika na kufanya kheri, na kujikalifu kufanya liwezekanalo, na kwamba kuna hisabu ya kuchungua kila kitu. Na mbali na hayo bado wanavyo vitendo vingine viovu wanavyo dumu navyo.


Arabic explanations of the Qur’an:

حَتَّىٰۤ إِذَاۤ أَخَذۡنَا مُتۡرَفِیهِم بِٱلۡعَذَابِ إِذَا هُمۡ یَجۡـَٔرُونَ ﴿٦٤﴾

Hata tutakapo watia katika adhabu wale walio dekezwa kwa starehe kati yao, hapo ndipo watapo yayatika.

Na Sisi tunapo wapatiliza adhabu matajiri wenye kudeka katika starehe zao hupiga makelele na wakayayatika kuomba msaada.


Arabic explanations of the Qur’an:

لَا تَجۡـَٔرُواْ ٱلۡیَوۡمَۖ إِنَّكُم مِّنَّا لَا تُنصَرُونَ ﴿٦٥﴾

Msiyayatike leo! Hakika nyinyi hamtanusurika nasi.

Basi tunawaambia: Msiyayatike, wala msiombe msaada hivi sasa. Hamtatoka ndani ya adhabu yangu, wala kuyayatika kwenu hakufai kitu.


Arabic explanations of the Qur’an:

قَدۡ كَانَتۡ ءَایَـٰتِی تُتۡلَىٰ عَلَیۡكُمۡ فَكُنتُمۡ عَلَىٰۤ أَعۡقَـٰبِكُمۡ تَنكِصُونَ ﴿٦٦﴾

Hakika zilikuwa Aya zangu mkisomewa, nanyi mkirudi nyuma juu ya visigino vyenu,

Hamna udhuru. Kwani Aya zangu zenye kuteremshwa kwa wahyi zilikuwa mkisomewa, nanyi mkizipuuza kwa mapuuza yenye kugeuza hali zenu, na wala hamkuzisadiki, wala hamkuzifuata kwa vitendo.


Arabic explanations of the Qur’an:

مُسۡتَكۡبِرِینَ بِهِۦ سَـٰمِرࣰا تَهۡجُرُونَ ﴿٦٧﴾

Na huku mkitakabari na usiku mkiizungumza (Qur'ani) kwa dharau.

Na nyinyi katika mapuuza yenu mlikuwa mnatakabari na mnafanyia maskhara, mkiutaja huu Wahyi kwa sifa mbaya mnapo kutana katika taanusi zenu za usiku.


Arabic explanations of the Qur’an:

أَفَلَمۡ یَدَّبَّرُواْ ٱلۡقَوۡلَ أَمۡ جَاۤءَهُم مَّا لَمۡ یَأۡتِ ءَابَاۤءَهُمُ ٱلۡأَوَّلِینَ ﴿٦٨﴾

Je, hawakuifikiri kauli, au yamewajia yasiyo wafikia baba zao wa zamani?

Je! Hawa wenye kupuuza wamekuwa wajinga hata hawakuizingatia Qur'ani wakaijua kwamba hii hakika ni Haki? Au huu wito wa Muhammad kwao umekuwa ni namna mbali kuliko walio kuja nayo Mitume wengine kwa kaumu zilizo kwisha tangulia walio ambao baba zao waliwawahi?


Arabic explanations of the Qur’an:

أَمۡ لَمۡ یَعۡرِفُواْ رَسُولَهُمۡ فَهُمۡ لَهُۥ مُنكِرُونَ ﴿٦٩﴾

Au hawakumjua Mtume wao, ndio maana wanamkataa?

Au hawamjui Mtume wao Muhammad aliye kulia kati yao katika tabia zake tukufu ambazo hazijapata kuwa na uwongo, na wao hivi sasa wanaukataa wito wake kwa dhulma na husda.


Arabic explanations of the Qur’an:

أَمۡ یَقُولُونَ بِهِۦ جِنَّةُۢۚ بَلۡ جَاۤءَهُم بِٱلۡحَقِّ وَأَكۡثَرُهُمۡ لِلۡحَقِّ كَـٰرِهُونَ ﴿٧٠﴾

Au wanasema: Ana wazimu? Bali amewajia kwa Haki, na wengi wao wanaichukia Haki.

Au wanasema kuwa huyu ni mwendawazimu? Hasha! Huyu hakika kawaletea Dini ya Haki, na wengi wao wanaichukia haki, kwani hiyo ni kinyume na matamanio yao na mapenzi yao, basi kwa hivyo hawamuamini.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَلَوِ ٱتَّبَعَ ٱلۡحَقُّ أَهۡوَاۤءَهُمۡ لَفَسَدَتِ ٱلسَّمَـٰوَ ٰ⁠تُ وَٱلۡأَرۡضُ وَمَن فِیهِنَّۚ بَلۡ أَتَیۡنَـٰهُم بِذِكۡرِهِمۡ فَهُمۡ عَن ذِكۡرِهِم مُّعۡرِضُونَ ﴿٧١﴾

Na lau kuwa Haki ingeli fuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na ardhi na waliomo ndani. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na ukumbusho wao.

Ingeli kuwa Haki inafuata matamanio yao ufisadi ungeli enea ulimwenguni, na hawa za nafsi zingeli pambana wenyewe kwa wenyewe. Lakini Sisi tumewapelekea Qur'ani ambayo inawakumbusha haki ambayo inapasa wote wajumuike juu yake. Na juu ya hivyo wao wanayapuuza hayo. "Na lau kuwa Haki ingeli fuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na ardhi na waliomo ndani. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na ukumbusho wao." Hilo neno "Haki" ni tamko lenye maana kadhaa. Huweza kuwa maana yake ni "Mwenyezi Mungu" Subhanahu wa Taa'la , mfano wa kauli yake Mtukufu: "Ametukuka Mwenyezi Mungu wa Haki". Pengine huwa maana yake ni "Qur'ani" , kwa mfano :"Hakika Sisi tumekutuma kwa Haki". Na huenda kukusudiwa "Dini yote", yaani miongoni mwake ni Qur'ani na Sunna (Hadithi) Sahihi, mfano wa kauli yake: "Na sema: Imekuja Haki na uwongo umetoweka". Na iliyo dhaahiri katika tamko la Haki hapa ni kuwa makusudio yake ni ile maana ya kwanza, yaani "Mwenyezi Mungu" Aliye takasika na kutukuka. Na kwa hivyo maana iliyo kusudiwa na Aya ni: Lau kuwa mwenendo wa Mwenyezi Mungu unafuatana na watakayo na wanayo yapendekeza makafiri mpango usingeli bakia katika hali iliyo simamia shani ya mpango wa mbingu na ardhi na wa viumbe viliomo ndani yake. Lakini Mwenyezi Mungu Mwenye hikima kuu na uwezo wa kutenda na ujuzi wake ulio enea kwa viumbe vyake na hikima yake ikadhamini kwa mpango madhubuti, na Qur'ani kusema kwa uwazi ya kwamba mbingu zina viumbe, anatuelekeza tufahamu: Kwanza kuwa Kuamini hayo kwa jumla ni yakini, tuache tafsili yake mpaka apendavyo Mwenyezi Mungu Subhanahu kuidhihirisha kwa kuambatana na kauli yake: "Tutawaonyesha Ishara zetu angani na katika nafsi zao." Pili: Anatuelekeza kwenye utafiti wa kisayansi kama tunaweza "kwani kufikilia hakika hii inatutilia nguvu Imani yetu. Na Imani ndiyo lengo muhimu katika kuelekea kwetu kwenye Ishara hizo."


Arabic explanations of the Qur’an:

أَمۡ تَسۡـَٔلُهُمۡ خَرۡجࣰا فَخَرَاجُ رَبِّكَ خَیۡرࣱۖ وَهُوَ خَیۡرُ ٱلرَّ ٰ⁠زِقِینَ ﴿٧٢﴾

Au unawaomba ujira? Lakini ujira wa Mola wako Mlezi ni bora, na Yeye ndiye Mbora wa wanao ruzuku.

Kwani, ewe Nabii! Unawataka ujira kwa huku kufikisha kwako ujumbe? Hayakuwa hayo! Kwa kuwa ujira hakika ujira wa Mola wako Mlezi ni bora zaidi kuliko walio nao wao; na Yeye ndiye Mbora wa kutoa.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَإِنَّكَ لَتَدۡعُوهُمۡ إِلَىٰ صِرَ ٰ⁠طࣲ مُّسۡتَقِیمࣲ ﴿٧٣﴾

Na kwa yakini wewe unawaita kwenye Njia Iliyo Nyooka.

Na hakika wewe, ewe Muhammad, hapana shaka yoyote unawaitia Dini ambayo ndiyo Njia Iliyo Nyooka yenye kupelekea Uwokovu.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَإِنَّ ٱلَّذِینَ لَا یُؤۡمِنُونَ بِٱلۡـَٔاخِرَةِ عَنِ ٱلصِّرَ ٰ⁠طِ لَنَـٰكِبُونَ ﴿٧٤﴾

Na hakika wale wasio iamini Akhera wanajitenga na Njia hiyo.

Na hakika hao wasio iamini Akhera na yalioko huko ya Pepo au Moto wanaiacha Njia Iliyo Nyooka inayo mhifadhi mpitaji wakaishika njia ya ubabaishi na misukosuko na ufisadi.


Arabic explanations of the Qur’an:

۞ وَلَوۡ رَحِمۡنَـٰهُمۡ وَكَشَفۡنَا مَا بِهِم مِّن ضُرࣲّ لَّلَجُّواْ فِی طُغۡیَـٰنِهِمۡ یَعۡمَهُونَ ﴿٧٥﴾

Na lau tungeli warehemu na tukawaondolea shida waliyo nayo bila ya shaka wangeli endelea katika upotofu wao vile vile, wakitangatanga.

Na lau tungeli warehemu, na tukawaondolea madhara yalio wateremkia katika miili yao, na ukame katika mali yao, na mfano wa hayo, basi hapana shaka yoyote wangeli zidi ukafiri, na wakaendelea katika maasi na jeuri.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَلَقَدۡ أَخَذۡنَـٰهُم بِٱلۡعَذَابِ فَمَا ٱسۡتَكَانُواْ لِرَبِّهِمۡ وَمَا یَتَضَرَّعُونَ ﴿٧٦﴾

Na hakika tuliwatia adhabu kali; lakini hawakuelekea kwa Mola wao Mlezi wala hawakunyenyekea.

Na Sisi kwa hakika tuliwapa adhabu kama kwa kuwauwa au kuwaletea njaa. Na wala hawakumnyenyekea Mola wao Mlezi, bali waliendelea na jeuri zao na kiburi chao kiasi ya kuondoka tu hiyo adhabu.


Arabic explanations of the Qur’an:

حَتَّىٰۤ إِذَا فَتَحۡنَا عَلَیۡهِم بَابࣰا ذَا عَذَابࣲ شَدِیدٍ إِذَا هُمۡ فِیهِ مُبۡلِسُونَ ﴿٧٧﴾

Mpaka tulipo wafungulia mlango wa adhabu kali, hapo ndipo wakawa wenye kukata tamaa.

Wanashikilia kupuuza kwao mpaka pale tunapo wapatiliza kwa adhabu kali ya njaa au mauwaji hapa duniani huwa tena wanababaika na kukata tamaa, hawaioni njia ya kuvuka.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَهُوَ ٱلَّذِیۤ أَنشَأَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَـٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَۚ قَلِیلࣰا مَّا تَشۡكُرُونَ ﴿٧٨﴾

Na Yeye ndiye aliye kuumbieni kusikia na kuona na nyoyo za kufahamu. Ni kuchache mno kushukuru kwenu.

Na yawaje mkamkufuri Mwenyezi Mungu na hali ni Yeye ndiye aliye kuumbieni usikizi mkaisikia Haki, aliye kupena uwezo wa kuona mkauona ulimwengu na viliomo ndani yake, na akakupeni akili mzingatie kwayo utukufu wake mpate kuamini? Hakika nyinyi hamumshukuru Mwenye kuumba vyote hivyo kwa Imani na ut'iifu ila kwa uchache tu, nao ni uchache mno!


Arabic explanations of the Qur’an:

وَهُوَ ٱلَّذِی ذَرَأَكُمۡ فِی ٱلۡأَرۡضِ وَإِلَیۡهِ تُحۡشَرُونَ ﴿٧٩﴾

Na Yeye ndiye aliye kuenezeni katika ardhi, na kwake Yeye mtakusanywa.

Na Yeye ndiye aliye kuumbeni duniani, na kwake Yeye peke yake ndio mtarejeshwa Siku ya Kiyama kwa ajili ya malipo.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَهُوَ ٱلَّذِی یُحۡیِۦ وَیُمِیتُ وَلَهُ ٱخۡتِلَـٰفُ ٱلَّیۡلِ وَٱلنَّهَارِۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ ﴿٨٠﴾

Na Yeye ndiye anaye huisha na kufisha, na yake Yeye mabadiliko ya usiku na mchana. Basi je! Hamfahamu?

Na Yeye ndiye anaye huisha na kufisha, na kwa amri yake na sharia zake ndio usiku na mchana zinapitishana. Na kukhitalifiana kwazo kwa urefu na ufupi, hamzingatii hiyo kuwa ni dalili ya uwezo wake na kupasa kumuamini Yeye na kuamini kufufuliwa? "Na Yeye ndiye anaye huisha na kufisha, na yake Yeye mabadiliko ya usiku na mchana. Basi je! Hamfahamu?" Aya zenye kutaja usiku na mchana zimekuja mwahala mwingi katika Qur'ani tukufu, na haya yanaonyesha kuwa Mwenyezi Mungu wa Haki, Aliye takasika na kutukuka, anawakumbusha waja wake kwa Ishara hii ya uumbaji; na kwa kuwa yamo maana ya ndani inawapelekea wenye kufikiri wazidi kuzingatia na kuchungua. Na kukhitalifiana usiku na mchana kunatokana na pande mbili kubwa: Kwanza: Kukhitalifiana kwa wakati, urefu na ufupi. Na Pili: Kukhitalifiana kwa dhaahiri ya tabia na isiyo onekana. Kwanza - Khitilafu kwa nyakati: Mchana ni kipindi cha wakati baina ya kudhihiri ncha ya jua na inapo potea upeo wa macho, pale linapoonekana kwa jicho kama linagusa uso wa ardhi. Na ilivyo kuwa kwa hakika pale pahali pake pa kuzama jua sipo hapo upeo wa macho, bali tunaona tu hivyo kwa kuwa miale inayo tokana na jua inapinda inapo pita katika matabaka ya anga mpaka inapo fikilia kwenye jicho la mtazamaji, na yeye akaliona jua kama lipo huko upeo wa macho. Lilio kweli ni kuwa kuzama huku kuko chini kuliko upeo wa macho kwa kadri ya dakika 35 kwa kipimo cha mduara. Na Usiku ni kipindi cha kutimiliza wakati wa mchana mpaka kitimilie kipindi cha mzunguko wa ardhi juu ya nafsi yake kutoka magharibi kwendea mashariki. Na baina ya Usiku na Mchana vipo vipindi viwili, navyo vya magharibi na mapambazuko. Na kipindi cha mchana kinakhitalifiana kwa mujibu wa hali ya uwazi wa pahala na musimu wa mwaka. Hali kadhaalika kipindi cha usiku kinakhitalifiana hivyo hivyo kwa kufuatana haya. Na nyakati za Swala na Saumu zinawekwa kufuatana na matulio ya jua huko upeo wa macho. Pili - Khitilafu katika yanayo dhihiri katika tabia: Na madhaahiri haya ni ya namna nyingi, na yanazalikana kutokana na michanganyiko ya miale ya jua, inayo onekana na isiyo onekana, na vitu vilio beba nguvu za umeme pamoja na vifuniko vya anga na nyuso za bahari na majangwa n.k. Kadhaalika yapo mambo ya kuonekana kama kupatwa kwa jua na mwezi, na nyota zenye kufanya mikia, nyota za dasturi na nyota ziendazo na mawingu meupe, na nyota zinazo anguka, na ambazo hufumbwa na ukali wa anga la jua kuonekana mchana, ilhali usiku huonekana wazi. Na muhimu kabisa katika yanayo onekana kuwa ni khitilafu baina ya usiku na mchana ni huu mwangaza wa mchana. Na sababu yake ni kuwa miale inayo toka kwenye jua inapo piga juu ya funiko la anga, ambalo kwa hakika ni sehemu ndogo ndogo zenye chembe chembe ndogo mno za vumbi, hizo hurejesha mwangaza na kuutawanya pande mbali mbali. Ikiwa hali ya anga ni safi, na vile vichembe chembe vya vumbi ni vidogo sana, na jua liko upeo wa macho, basi rangi inayo enea zaidi na inayo onekana kwa macho zaidi, inakuwa ya kibuluu. Ama wakati wa kuchomoza jua au kuchwa basi mbingu huonekana na rangi ya machungwa yenye kupiga wekundu, na mwangu wa kibuluu unatawanyika. Nz kwa hivyo mbingu utosini huelekea kuwa kibuluu khafifu. Na wakati wa kuchwa jua tunaona rangi ya kijani kiasi ya nukta moja hivi au akali pembezoni mwake. Huu huitwa mmetuko wa kijani, na aghlabu yake huonekana unapo kuwa baharini, au nyuma ya kilele cha mlima, au hata kwenye kuta za majumba. Na asli ya kuonekana hivi ni kwa ajili ya kugeuka na kutawanyika miale ya jua hata ikatoa rangi mbali mbali katika hizo kijani. Mukhtasari wa haya ni kuwa miale ya jua ina rangi zinazo onekana na zisizo onekana. Na zinakhitalifiana kwa urefu wa mawimbi yake na kufuata kwake sifa hiyo. Kwa hivyo ndio tunaona kwa migongano hiyo mwangaza wa mchana, mazigazi (sarabi), upinde wa mvua, na rangi za aina mbali mbali zinazo zunguka jua, na mengineyo katika Ishara za mbinguni za ulimwengu tuuonao. Na linapo potea jua jioni mbingu inaonekana kwa rangi mbali mbali kwa sababu ya kuparaganyika mwangaza katika matabaka ya anga la juu. Na kila jua likiteremka unapungua mwangaza wa jioni, na zinapungua zile rangi zake za tabia, mpaka likifikilia daraja ya duara 18.5 mbingu inakuwa kiza. Na wataalamu wa nyakati wameweka kuwa huu ndio wakati wa kuambiwa kuwa usiku umekuwa giza na kwa hivyo ndio wakati wa kuadhinia Sala ya Isha. Na wakati huo khasa ndio huanza mwangaza wa nyota kama sura ya mnara wa sukari na tako lake liko upeo wa magharibi. Na hivyo huendelea katika masiku safi ya siku za baridi mpaka kilele cha ile "cone" au "makhruut'" yaani sura ya mnara wa sukari kifikie utosini. Na kati kati ya usiku hudhihiri rangi za kuchomoza jua kidogo kidogo wakati wa mapambazuko kwanza kama kilele cha ile "cone" au "makhruut'" . Kilele chake hicho huzidi kupanda , na tako lake hutanuka kwenye upeo wa mashariki mpaka inapo dhihiri alfajiri, yaani linapo kuwa jua liko chini ya upeo wa macho wa mashariki kwa kadri ya daraja 18.5 za duara. Na hapo ndio wakati wa kuadhiniwa Swala ya Alfajiri. Na rangi za mapambazuko huanza kudhihiri kwa taratibu kinyume na zile za kuchwea jua magharibi. Na imedhihiri karibuni kuwa jua lina kifuniko chembamba kimetanda angani takriban kimekaribia kufunika anga lote la ardhi. Kifuniko hichi chembemba ndicho kinacho sabibisha kuleta rangi mbali mbali za katika anga. Mambo haya mbali mbali ambayo tumeyataja kama ni mifano isiyo na ukomo imetuonyesha vipi mbingu inavyo kuwa pindi ikiwa hapana mawingu wala hapana pepo za mchanga. Kwani hapo tena huwa ni kiza. Na ikiwa mawingu yamebeba matone ya maji ya mvua basi hayo hupambana na miale ya jua, na hufanyika kama huo upinde wa mvua katika hali maalumu. Na ikiwa mawingu yenyewe ni ya namna fulani ambayo yanabeba maji yaliyo ganda (crystals) "kristali" zenye pande sita, basi maji hayo huingiana na miale ya jua na hiyo miale huvunjika ndani ya hayo maji (kama mwaangaza upitavyo katika kigae cha thuraya, "prism") kisha mwangaza huo ukatoka nje kwa rangi mbali mbali. Na katika hali fulani fulani ndio hutokea rangi nzuri nzuri kulizunguka jua. Na wakati wa weusi wa usiku utaziona nyota kama kwamba zipo karibu nasi na kwa hakika hizo ziko mbali kwa masafa makubwa sana ya kukisiwa kwa miaka na miaka ya mwendo wa mwanga. Vile vile tunaona katika anga hili nyota na sayari na nyota mkia na vimondo kama kwamba zipo karibu, utadhani kuwa khitilafu ya masafa imeondoka kabisa. Na haya ndiyo yanayo tupelekea tutambue maana iliyo fichikana ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na tumeifanya mbingu kama dari iliyo hifadhiwa; nao wamezipuuza Ishara zetu." Kama tulivyo kwisha eleza kuwa juu ya miale inayo tokana na jua kuna miale inayo tokana na vitu vingine vya eneo la jua vyenye nishat'i ya nguvu, na vyenye kubeba nguvu za umeme. Kadhaalika inatokana na hizo miale iliyo juu ya zambarau Ultra Violet Rays. Vitu hivi na miale hii inapambana na matabaka ya anga la juu, na huathirika kwa mvuto wa smaku kuizunguka dunia. Kwa hivyo hulitibua anga la kaskazini na kusini, na huleta kiza katika mbingu ya kaskaazini kama kwamba ni pazia kuzuia mianga yenye rangi nzuri nzuri za kijani zenye kumili kwenye wekundu na kibuluu. Sura hizi hubaki pengine muda wa saa kadhaa katika mbingu ya kaskazini, na zaidi waweza kuziona masiku kadhaa wa kadhaa linapo kuwa jua linashitadi. Mapazia haya si kama unayaona kaskazini tu, bali hata pia katika kati kati ya dunia. Na katika mbingu vipo vibebaji nguvu za umeme katika mawingu na anga ambavyo huzalikana kutokana navyo radi na mimetuko katika anga la juu. Mambo yote haya yanayo onekana ambayo tunayashuhudia yanatupelekea tufahama maana ya ndani ya kauli yake Subhanahu wa Taa'la: "Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi na kukhitalifana usiku na mchana pana Ishara kwa wenye akili." Kutokana na yaliyo pita kwa mambo ya dhaahiri ya maumbile inabainikana kwamba haya yanakuwa kwa sababu ambazo hayumkini mwanaadamu kuingilia ndani yake. Na hakika ni Mwenyezi Mungu, Aliye tukuka shani yake, ndiye mwenye kuleta hizo khitilafu za usiku na mchana, wala hawezi binaadamu kabisa siku yoyote kuweza kugeuza usiku wala mchana. Na Yeye Mwenyezi Mungu Aliye tukuka shani yake ndiye anaye zifuatanisha usiku na mchana kwa mizani madhubuti na vipimo baraabara, na anaendesha siku zote mwaka ingia mwaka toka.


Arabic explanations of the Qur’an:

بَلۡ قَالُواْ مِثۡلَ مَا قَالَ ٱلۡأَوَّلُونَ ﴿٨١﴾

Bali wanasema kama walivyo sema watu wa kwanza.

Hawakuzingatia hayo, bali waliwafuata wakanushaji walio kwisha tangulia, wakasema kama walivyo sema hao.


Arabic explanations of the Qur’an:

قَالُوۤاْ أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابࣰا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ ﴿٨٢﴾

Walisema: Je! Tukisha kufa tukawa udongo na mifupa ndio tutafufuliwa?

Katika kukanusha kwao kufufuliwa, walisema: Hivyo sisi tutafufuliwa baada ya kwisha geuka mchanga na mifupa?


Arabic explanations of the Qur’an:

لَقَدۡ وُعِدۡنَا نَحۡنُ وَءَابَاۤؤُنَا هَـٰذَا مِن قَبۡلُ إِنۡ هَـٰذَاۤ إِلَّاۤ أَسَـٰطِیرُ ٱلۡأَوَّلِینَ ﴿٨٣﴾

Tuliahidiwa haya sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni visa vya uwongo vya watu wa zamani.

Sisi tuliahidiwa haya, na pia baba zetu waliahidiwa hayo hayo hapo zamani. Haya si chochote ila ni ahadi za uwongo walizo buni watu wa zamani.


Arabic explanations of the Qur’an:

قُل لِّمَنِ ٱلۡأَرۡضُ وَمَن فِیهَاۤ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ ﴿٨٤﴾

Sema: Ni ya nani ardhi na viliomo ndani yake, kama nyinyi mnajua?

Ewe Muhammad! Waambie: Ni nani aliye imiliki ardhi na viliomo ndani yake, tangu watu mpaka viumbe vyote? Kama nyinyi mna ujuzi nijibuni.


Arabic explanations of the Qur’an:

سَیَقُولُونَ لِلَّهِۚ قُلۡ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿٨٥﴾

Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu! Sema: Basi, je, hamkumbuki?

Watakiri kuwa ardhi ni ya Mwenyezi Mungu. Basi hapo tena waambie: Hamkumbuki kuwa Mwenye kumiliki hayo ndiye anaye faa kuabudiwa peke yake?


Arabic explanations of the Qur’an:

قُلۡ مَن رَّبُّ ٱلسَّمَـٰوَ ٰ⁠تِ ٱلسَّبۡعِ وَرَبُّ ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡعَظِیمِ ﴿٨٦﴾

Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu saba na Mola Mlezi wa A'rshi Kuu?

Waambie tena: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu saba na Mola Mlezi wa A'rshi Kuu? (Kiti Kikuu cha Enzi)


Arabic explanations of the Qur’an:

سَیَقُولُونَ لِلَّهِۚ قُلۡ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٨٧﴾

Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, hamwogopi?

Watakiri kuwa huyo ni Mwenyezi Mungu. Basi waambie: Je! Hamwogopi matokeo ya ushirikina wenu na ukafiri wenu na kumuasi kwenu Mwenye uumbaji huu wote mkubwa?


Arabic explanations of the Qur’an:

قُلۡ مَنۢ بِیَدِهِۦ مَلَكُوتُ كُلِّ شَیۡءࣲ وَهُوَ یُجِیرُ وَلَا یُجَارُ عَلَیۡهِ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ ﴿٨٨﴾

Sema: Ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu, naye ndiye anaye linda, wala hakilindwi asicho taka, kama mnajua?

Waambie vile vile: Nani mwenye ufalme wa kila kitu mkononi mwake, na mwenye madaraka yasio na ukomo katika kila kitu, na ambaye ndiye kwa uwezo wake analinda kila kitu, wala hayamkiniki yeyote kumlinda yeyote na adhabu yake? Kama nyinyi mnaijua jawabu, basi nijibuni.


Arabic explanations of the Qur’an:

سَیَقُولُونَ لِلَّهِۚ قُلۡ فَأَنَّىٰ تُسۡحَرُونَ ﴿٨٩﴾

Watasema: (Ufalme huo) ni wa Mwenyezi Mungu. Sema: Basi vipi mnadanganyika?

Watakiri kuwa hakika huyo ni Mwenyezi Mungu. Waambie: Basi huwaje mkadanganyika kwa pumbao na kuchochewa na mashetani, na mkaacha ut'iifu wa Mwenyezi Mungu?


Arabic explanations of the Qur’an:

بَلۡ أَتَیۡنَـٰهُم بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّهُمۡ لَكَـٰذِبُونَ ﴿٩٠﴾

Bali tumewaletea Haki, na kwa yakini hao ni waongo.

Hakika Sisi tumewabainishia Haki kwa ndimi za Mitume, na wao ni waongo katika kila jambo linalo khitalifu na Haki hii.


Arabic explanations of the Qur’an:

مَا ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ مِن وَلَدࣲ وَمَا كَانَ مَعَهُۥ مِنۡ إِلَـٰهٍۚ إِذࣰا لَّذَهَبَ كُلُّ إِلَـٰهِۭ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضࣲۚ سُبۡحَـٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا یَصِفُونَ ﴿٩١﴾

Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Inge kuwa hivyo basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu.

Mwenyezi Mungu hakumchukua yeyote kuwa ni mwanawe. Yeye ametakasikia na hayo. Wala hana mshirika. Angeli kuwa na mshirika basi kila mmoja wao angejipa madaraka ya pekee kwa alivyo viumba, na vikawa ndio milki yake, na wangeli gombana wenyewe kwa wenyewe kama wanavyo onekana wafalme wanavyo fanya. Na ulimwengu ungeli fisidika kwa mizozano hiyo. Basi Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wayasemayo washirikina yanayo kwenda kinyume na Haki.


Arabic explanations of the Qur’an:

عَـٰلِمِ ٱلۡغَیۡبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ فَتَعَـٰلَىٰ عَمَّا یُشۡرِكُونَ ﴿٩٢﴾

Mjuzi wa siri na dhaahiri, na ametukuka juu ya hayo wanayo mshirikisha nayo.

Na Yeye amevizunguka vitu vyote kwa kuvijua. Anajua tusiyo yaona na tunayo yaona. Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wanayo mnasibisha nayo makafiri kuwa ati ana washirika.


Arabic explanations of the Qur’an:

قُل رَّبِّ إِمَّا تُرِیَنِّی مَا یُوعَدُونَ ﴿٩٣﴾

Sema: Mola wangu Mlezi! Ukinionyesha adhabu waliyo ahidiwa,

Ewe Nabii! Sema: Ukiwateremshia adhabu ulio waahidi hapa duniani nami nipo pamoja nao,


Arabic explanations of the Qur’an:

رَبِّ فَلَا تَجۡعَلۡنِی فِی ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّـٰلِمِینَ ﴿٩٤﴾

Mola wangu Mlezi! Usinijaalie katika watu madhaalimu hao.

Basi nakuomba usinifanye mwenye kuadhibiwa pamoja na makafiri waasi.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَإِنَّا عَلَىٰۤ أَن نُّرِیَكَ مَا نَعِدُهُمۡ لَقَـٰدِرُونَ ﴿٩٥﴾

Na hakika Sisi ni waweza wa kukuonyeshsa tuliyo waahidi.

Na Sisi tunaweza kwa utimilivu kukuonyesha adhabu tulio waahidi ikiwateremkia. Basi wewe tuwa ujue kuwa tutashinda.


Arabic explanations of the Qur’an:

ٱدۡفَعۡ بِٱلَّتِی هِیَ أَحۡسَنُ ٱلسَّیِّئَةَۚ نَحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا یَصِفُونَ ﴿٩٦﴾

Kinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi. Sisi tunajua wayasemayo.

Wewe endelea na wito wako, na ukabili uovu wao kwa vitendo vilivyo vizuri kama kusamehe au vyenginevyo. Na Sisi tunajua vyema wanakutaja vipi wewe, na wanavyo usema kwa ubaya huo wito wako kwa uwovu na uzushi. Na Sisi tutawalipa kwa hayo.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنۡ هَمَزَ ٰ⁠تِ ٱلشَّیَـٰطِینِ ﴿٩٧﴾

Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani.

Nawe sema: Ewe Mola Mlezi! Najilinda kwako na wasiwasi wa mashetani wasiniingilie katika nafsi yangu kwa vitendo visio kupendeza.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن یَحۡضُرُونِ ﴿٩٨﴾

Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie.

Na ewe Mola Mlezi! Najilinda kwako wasiwe nami katika kitendo chochote ili kitendo hicho kiwe kimetakasika, safi, kwa ajili ya ridhaa yako tukufu.


Arabic explanations of the Qur’an:

حَتَّىٰۤ إِذَا جَاۤءَ أَحَدَهُمُ ٱلۡمَوۡتُ قَالَ رَبِّ ٱرۡجِعُونِ ﴿٩٩﴾

Mpaka yanapo mfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe.

Wanaendelea kuwakanusha mpaka utapo fika wakati wa kufa mmoja wao hujuta na akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nirudishe duniani.


Arabic explanations of the Qur’an:

لَعَلِّیۤ أَعۡمَلُ صَـٰلِحࣰا فِیمَا تَرَكۡتُۚ كَلَّاۤۚ إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَاۤىِٕلُهَاۖ وَمِن وَرَاۤىِٕهِم بَرۡزَخٌ إِلَىٰ یَوۡمِ یُبۡعَثُونَ ﴿١٠٠﴾

Ili nitende mema sasa badala ya yale niliyo yaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watapo fufuliwa.

Ili nipate kufanya a'mali njema katika mali au wakati nilio acha. Wala ombi lake halitokubaliwa. Kwani haya ni maneno anayasema bila ya faida, hayakubaliwi. Na pindi akikubaliwa hatotenda kitu. Na juu ya yote hatorudi kabisa! Kwani mauti ni kizuizi baina yao na hayo wanayo yatamani mpaka Mwenyezi Mungu atapo wafufua.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَإِذَا نُفِخَ فِی ٱلصُّورِ فَلَاۤ أَنسَابَ بَیۡنَهُمۡ یَوۡمَىِٕذࣲ وَلَا یَتَسَاۤءَلُونَ ﴿١٠١﴾

Basi litapo pulizwa baragumu hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana.

Ukifika wakati wa kufufuliwa tutawafufua kutoka makaburini kwao. Na hayo ni kwa mfano wa kupulizwa tarumbeta watafufuka nao wamefarikiana. Hapana mtu utaomfaa ujamaa wake na fulani. (Ujamaa Kiswahili maana yake makhusiano ya nasaba, sio usoshalisti.) Wala hapana mtu atae muomba mtu kitu cha kumfaa. Kwani kila mmoja wao siku hiyo atakuwa kashughulika na lake.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَمَن ثَقُلَتۡ مَوَ ٰ⁠زِینُهُۥ فَأُوْلَـٰۤىِٕكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ ﴿١٠٢﴾

Ama wale ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio wenye kufanikiwa.

A'mali (Vitendo) ndio mizani ya kupimia. Mwenye Imani nzuri na vitendo vyema atakuwa na uzito katika mizani ya Mwenyezi Mungu. Hao ndio walio fuzu.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَمَنۡ خَفَّتۡ مَوَ ٰ⁠زِینُهُۥ فَأُوْلَـٰۤىِٕكَ ٱلَّذِینَ خَسِرُوۤاْ أَنفُسَهُمۡ فِی جَهَنَّمَ خَـٰلِدُونَ ﴿١٠٣﴾

Na wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi, hao ndio walio zitia khasarani nafsi zao, na katika Jahannamu watadumu.

Na asiye kuwa na thawabu au vitendo vyenye uzito mbele ya Mwenyezi Mungu, hao ndio walio zikhasiri nafsi zao kwa kuziuza kwa Shetani. Nao wataadhibiwa Motoni, wadumu humo.


Arabic explanations of the Qur’an:

تَلۡفَحُ وُجُوهَهُمُ ٱلنَّارُ وَهُمۡ فِیهَا كَـٰلِحُونَ ﴿١٠٤﴾

Moto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizo kunjana.

Moto utawababua nyuso zao, nazo zitakuwa zimekunjana kwa uwovu wa mwisho wao.


Arabic explanations of the Qur’an:

أَلَمۡ تَكُنۡ ءَایَـٰتِی تُتۡلَىٰ عَلَیۡكُمۡ فَكُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ ﴿١٠٥﴾

Je! Hazikuwa Aya zangu mkisomewa, na nyinyi mkizikanusha?.

Mwenyezi Mungu anawakemea na anawaambia: Aya zangu zilizo kuwa zinateremshwa zilikuwa mkisomewa duniani, nanyi mkizikadhibisha.


Arabic explanations of the Qur’an:

قَالُواْ رَبَّنَا غَلَبَتۡ عَلَیۡنَا شِقۡوَتُنَا وَكُنَّا قَوۡمࣰا ضَاۤلِّینَ ﴿١٠٦﴾

Mola wetu Mlezi! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa watu tulio potea.

Watasema nao wanakiri makosa yao : Ewe Mola wetu Mlezi! Maasi yetu yalikuwa mengi, ndio yakatupatia mashaka, na tukawa wenye kupotea tukaiacha njia ya sawa.


Arabic explanations of the Qur’an:

رَبَّنَاۤ أَخۡرِجۡنَا مِنۡهَا فَإِنۡ عُدۡنَا فَإِنَّا ظَـٰلِمُونَ ﴿١٠٧﴾

Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tufanyapo tena basi kweli sisi ni wenye kudhulumu.

Na watasema: Mola wetu Mlezi! Tutoe Motoni na uturejeshe duniani. Basi tukirudi tena kwenye ukafiri na uasi basi tutakuwa kweli ni twenye kujidhulumu nafsi zetu.


Arabic explanations of the Qur’an:

قَالَ ٱخۡسَـُٔواْ فِیهَا وَلَا تُكَلِّمُونِ ﴿١٠٨﴾

Atasema Mwenyezi Mungu: Tokomeeni humo, wala msinisemeze.

Na Mwenyezi Mungu atawaambia kwa kuwadharau na kuwabeza: Kaeni humo kwa madhila na unyonge, wala msiseme nami kabisa!


Arabic explanations of the Qur’an:

إِنَّهُۥ كَانَ فَرِیقࣱ مِّنۡ عِبَادِی یَقُولُونَ رَبَّنَاۤ ءَامَنَّا فَٱغۡفِرۡ لَنَا وَٱرۡحَمۡنَا وَأَنتَ خَیۡرُ ٱلرَّ ٰ⁠حِمِینَ ﴿١٠٩﴾

Bila ya shaka lilikuwapo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanao rehemu.

Mimi sikukudhulumuni, bali nyinyi mmejidhulumu wenyewe. Kwani Waumini wema katika waja wangu walikuwa wakisema duniani: Ewe Mola wetu Mlezi! Tumeamini. Basi tughufirie na uturehemu. Na Wewe ndiwe Mbora wa wanao rehemu.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَٱتَّخَذۡتُمُوهُمۡ سِخۡرِیًّا حَتَّىٰۤ أَنسَوۡكُمۡ ذِكۡرِی وَكُنتُم مِّنۡهُمۡ تَضۡحَكُونَ ﴿١١٠﴾

Lakini nyinyi mliwakejeli hata wakakusahaulisheni kunikumbuka, na mlikuwa mkiwacheka.

Na nyinyi daima mlikuwa mkiwafanyia maskhara, mpaka maskhara yenu yakakusahaulisheni kunikumbuka Mimi na kuniabudu Mimi. Basi hamkuamini wala hamkut'ii. Nanyi mlikuwa mkiwacheka kwa kejeli.


Arabic explanations of the Qur’an:

إِنِّی جَزَیۡتُهُمُ ٱلۡیَوۡمَ بِمَا صَبَرُوۤاْ أَنَّهُمۡ هُمُ ٱلۡفَاۤىِٕزُونَ ﴿١١١﴾

Hakika Mimi leo nimewalipa kwa vile walivyo subiri. Bila ya shaka hao ndio wenye kufuzu.

Hakika Mimi hii leo nimewalipa wao kwa mafanikio, kwa kuwa waliyavumilia maskhara yenu na maudhi yenu.


Arabic explanations of the Qur’an:

قَـٰلَ كَمۡ لَبِثۡتُمۡ فِی ٱلۡأَرۡضِ عَدَدَ سِنِینَ ﴿١١٢﴾

Atasema: Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hisabu ya miaka?.

Mwenyezi Mungu atawaambia makafiri: Mliishi miaka mingapi huko duniani?


Arabic explanations of the Qur’an:

قَالُواْ لَبِثۡنَا یَوۡمًا أَوۡ بَعۡضَ یَوۡمࣲ فَسۡـَٔلِ ٱلۡعَاۤدِّینَ ﴿١١٣﴾

Watasema: Tulikaa siku moja au sehemu ya siku. Basi waulize wanao weka hisabu.

Watasema kwa kuyaona mafupi maisha yao kwa adhabu wanayo ikuta: Tuliishi muda wa siku moja au baadhi ya siku hivi. Basi waulize wanao weza kuhisabu, sisi tumeshughulishwa na hii adhabu.


Arabic explanations of the Qur’an:

قَـٰلَ إِن لَّبِثۡتُمۡ إِلَّا قَلِیلࣰاۖ لَّوۡ أَنَّكُمۡ كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ ﴿١١٤﴾

Atasema: Nyinyi hamkukaa huko duniani ila kidogo, laiti ingeli kuwa mnajua.

Basi Mwenyezi Mungu atawaambia: Hamkuishi duniani ila muda mchache tu. Na lau ingeli kuwa mnajua malipo ya ukafiri na uasi na kwamba starehe ya duniani ni chache mngeli amini na mkat'ii.


Arabic explanations of the Qur’an:

أَفَحَسِبۡتُمۡ أَنَّمَا خَلَقۡنَـٰكُمۡ عَبَثࣰا وَأَنَّكُمۡ إِلَیۡنَا لَا تُرۡجَعُونَ ﴿١١٥﴾

Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?.

Je? Mlidhani kuwa tuliwaumbeni bila ya hikma, ndio mukafanya ufisadi katika ardhi, na mkadhani kuwa hamtafufuliwa mpate kulipwa.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَتَعَـٰلَى ٱللَّهُ ٱلۡمَلِكُ ٱلۡحَقُّۖ لَاۤ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡكَرِیمِ ﴿١١٦﴾

Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki, hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi Tukufu.

Utukufu ni wa Mwenyezi Mungu peke yake. Na Yeye ndiye Mwenye kumiliki ufalme wote. Hapana Mwenye kuabudiwa kwa Haki isipo kuwa Yeye. Na Yeye ndiye Mwenye A'rshi Tukufu.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَمَن یَدۡعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ لَا بُرۡهَـٰنَ لَهُۥ بِهِۦ فَإِنَّمَا حِسَابُهُۥ عِندَ رَبِّهِۦۤۚ إِنَّهُۥ لَا یُفۡلِحُ ٱلۡكَـٰفِرُونَ ﴿١١٧﴾

Na anaye muomba - pamoja na Mwenyezi Mungu - mungu mwenginewe hana ushahidi wa hili; basi bila ya shaka hisabu yake iko kwa Mola wake Mlezi. Kwa hakika makafiri hawafanikiwi.

Na mwenye kumuabudu mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu hana ushahidi wa kumfanya huyo astahiki kuabudiwa. Hakika Mwenyezi Mungu atampa adhabu kwa ushirikina wake bila ya shaka yoyote. Hakika makafiri hawaongokewi. Bali watao ongokewa ni Waumini.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَقُل رَّبِّ ٱغۡفِرۡ وَٱرۡحَمۡ وَأَنتَ خَیۡرُ ٱلرَّ ٰ⁠حِمِینَ ﴿١١٨﴾

Nawe sema: Mola wangu Mlezi! Samehe na urehemu nawe ni Mbora wa wanao rehemu.

Na sema, ewe Nabii, ukimlingania Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea: Ewe Mola wangu Mlezi! Nisamehe dhambi zangu, na nirehemu. Kwani Wewe ni Mbora wa wanao rehemu, kwa sababu rehema yako imeenea na ipo karibu kwa watendao mema.


Arabic explanations of the Qur’an: