Surah At-Tin (The Fig)

Listen

Swahili

Surah At-Tin (The Fig) - Aya count 8

بِّسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِیمِ وَٱلتِّینِ وَٱلزَّیۡتُونِ ﴿١﴾

Naapa kwa tini na zaituni!

Naapa kwa tini na zaituni, kwa baraka zao na ubora wa manufaa yao.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَطُورِ سِینِینَ ﴿٢﴾

Na kwa Mlima wa Sinai!

Na kwa mlima ambao juu yake ndio Mwenyezi Mungu alimsemeza Musa.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَهَـٰذَا ٱلۡبَلَدِ ٱلۡأَمِینِ ﴿٣﴾

Na kwa mji huu wenye amani!

Na kwa huu mji mtukufu wa Makka, ambao anaushuhudia utukufu wake mwenye kwenda uzuru, na anapata amani mwenye kuuingia.


Arabic explanations of the Qur’an:

لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ فِیۤ أَحۡسَنِ تَقۡوِیمࣲ ﴿٤﴾

Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.

Kwa hakika bila ya shaka yoyote Sisi tumemuumba mtu amesimama sawa kwa umbo bora kabisa lilio nyooka, na akasifika kwa sifa nzuri kabisa.


Arabic explanations of the Qur’an:

ثُمَّ رَدَدۡنَـٰهُ أَسۡفَلَ سَـٰفِلِینَ ﴿٥﴾

Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!

Kisha tukamteremsha cheo mpaka akawa ni wa chini kabisa katika hao walioko chini, kwa kuacha kufanya waajibu wa hayo tuliyo muumbia.


Arabic explanations of the Qur’an:

إِلَّا ٱلَّذِینَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ فَلَهُمۡ أَجۡرٌ غَیۡرُ مَمۡنُونࣲ ﴿٦﴾

Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha.

Lakini walio amini na wakatenda vitendo vyema, hao basi watapata ujira usio wakatikia wala kuwapungukia.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَمَا یُكَذِّبُكَ بَعۡدُ بِٱلدِّینِ ﴿٧﴾

Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo?

Basi kitu gani kinacho kupelekea kukadhibisha kufufuliwa na kulipwa baada ya kuwekwa wazi uweza wetu wa hayo?


Arabic explanations of the Qur’an:

أَلَیۡسَ ٱللَّهُ بِأَحۡكَمِ ٱلۡحَـٰكِمِینَ ﴿٨﴾

Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?

Kwani Mwenyezi Mungu aliye yatenda hayo tuliyo kueleza si muadilifu kuliko mahakimu wote kwa kufanya na kupanga?


Arabic explanations of the Qur’an: