Surah Az-Zalzalah (The Earthquake)

Listen

Swahili

Surah Az-Zalzalah (The Earthquake) - Aya count 8

إِذَا زُلۡزِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ زِلۡزَالَهَا ﴿١﴾

Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!

Ikitisika ardhi kwa mtikiso mkubwa, na ikasukika kwa ukomo wa kutisika na kusukika kunako mkinika na ikaweza kuchukua!


Arabic explanations of the Qur’an:

وَأَخۡرَجَتِ ٱلۡأَرۡضُ أَثۡقَالَهَا ﴿٢﴾

Na itakapo toa ardhi mizigo yake!

Na ardhi ikatoa yote yaliomo katika ndani ya tumbo lake, ikiwa khazina au maiti walio kwisha zikwa!


Arabic explanations of the Qur’an:

وَقَالَ ٱلۡإِنسَـٰنُ مَا لَهَا ﴿٣﴾

Na mtu akasema: Ina nini?

Na binaadamu akasema kwa kushtuka na khofu: Ardhi hii ina nini hata inatikisika hivi, na inatoa vilivyomo tumboni mwake, ndio Saa imefika?


Arabic explanations of the Qur’an:

یَوۡمَىِٕذࣲ تُحَدِّثُ أَخۡبَارَهَا ﴿٤﴾

Siku hiyo itahadithia khabari zake.

Siku hiyo ardhi itamsimulia mtu khabari zake zilio mshitua,


Arabic explanations of the Qur’an:

بِأَنَّ رَبَّكَ أَوۡحَىٰ لَهَا ﴿٥﴾

Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!

Kwani Mlezi wake na Muumba wake atakuwa kaifunulia, kaipa Wahyi, na kaiamuru itetemeke na ijisuke suke, ndio ikafanya upesi kutekeleza amri.


Arabic explanations of the Qur’an:

یَوۡمَىِٕذࣲ یَصۡدُرُ ٱلنَّاسُ أَشۡتَاتࣰا لِّیُرَوۡاْ أَعۡمَـٰلَهُمۡ ﴿٦﴾

Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!

Siku hiyo watu watatoka makaburini mbio, nao wamo katika mtafaruku, wapate kuziona hisabu zao na malipo yao aliyo waahidi Mwenyezi Mungu.


Arabic explanations of the Qur’an:

فَمَن یَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٍ خَیۡرࣰا یَرَهُۥ ﴿٧﴾

Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona!

Basi mwenye kufanya hata kitu chenye uzito wa punje ya mchanga cha kheri ataiona katika daftari lake, na atapata malipo yake.


Arabic explanations of the Qur’an:

وَمَن یَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةࣲ شَرࣰّا یَرَهُۥ ﴿٨﴾

Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!

Na mwenye kufanya shari ya uzito wa chembe ya mchanga ataiona kadhaalika, na atapata malipo yake. Wala Mola wako Mlezi hatamdhulumu yeyote.


Arabic explanations of the Qur’an: